Skip to main content

Mkuu wa haki za binadamu itaka Indonesia kusitisha unyongaji

Mkuu wa haki za binadamu itaka Indonesia kusitisha unyongaji

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein leo Jumatano ameelezea hofu yake kuhusu ripoti kwamba watu wapatao 14 wanakabiliwa na hukumu ya kunyongwa nchini Indonesia , wengi wao kwa makossa yanayohusiana na mihadarati.

Zeid ametoa wito kwa mamlaka ya serikali kusitisha mara moja huku ya kifo. Unyongaji huo unatarajiwa kufanyika wiki hii katika gereza lenye ulinzi mkali la kisiwani Nusa Kambangan katikati mwa jimbo la Java.

Pia ofisi ya haki za binadamu imeelezea wasiwasi wake kuhusu kutokuwepo na uwazi katika mchakato mzima wa  kutozingatiwa kwa haki katika kesi, ikiwa ni pamoja na haki ya kukata rufaa. Zeid amesema kuendelea kutumia hukumu ya kifo Indonesia kunatia hofu na ameitaka serikali kukomesha hukumu hizo na kuzingatia haki za binadamu. Tangu mwaka 2013 watu 19 wameshanyongwa , na kulifanya taiafa hilo kuwa mnyongaji mkubwa zaidi Kusini Mashariki mwa Asia.