Skip to main content

Ban alaani shambulio nchini Afghanistan aliita la kupuuzwa

Ban alaani shambulio nchini Afghanistan aliita la kupuuzwa

Umoja wa Mataifa umelaani shambulio lililosababisha vifo vya watu 80 na kujeruhi zaidi ya 200 mjini Kabul nchini Afghanistan.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio hilo lililotekelezwa jumamosi akiliita ni uhalifu wa kupuuzwa huku pia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likilaani shambulio hilo.

Kundi la kigaidi ISIL au Daesh limekiri kuhusika na shambulio hilo kupitia washirika wao wa vyombo vya habari.

Milipuko miwili ilitokea mjini Kabul wakati maelfu ya watu wengi wao wakiwa ni jamii ndogo ya Hazara, wakiandamana kupinga uwepo wa mkondo wa umeme katika eneo lao.