Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mapigano Mali

Ban alaani mapigano Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mapigano kati ya vikundi viwili vyenye silaha Kaskazini mwa Mali, vikundi ambavyo vilitia saini makubaliano ya amani yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa waka mmoja uliopita.

Katika taarifa, Ban amesema amesikitishwa na machafuko na kuongeza kuwa siku mbili za mapigano mjini Kidal zimteshia kufuta uanzishwaji wa mamlaka sawia katika ukanda huo.

Ban ameungana na ujumbe wa UM nchini Mali MINUSAMA, akitaka

vikundi hivyo kinzani kusitisha uhasama hima na kurejesha hali ya amani mjini hapo.

Amesema wakati huu mchakato wa amani ukiendela, pande zote zilizosaini zilipaswa kuchukua hatua muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa mchakato huo ikiwamo kuunda mamlaka za mpito na mipango ya kiusalama.

Serikali ya Mali imetangaza siku za hali ya dharura na kipindi cha maombolezo ya kitaifa baada ya wanajeshi 17 kuuliwa na wengine 35 kujeruhiwa baada ya shambulio katika kituo cha kijeshi kati mwa nchi hiyo.