Skip to main content

Baraza lataka mchakato wa uchaguzi DR Congo kuzingatia katiba

Baraza lataka mchakato wa uchaguzi DR Congo kuzingatia katiba

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limesisitiza umuhimu wa kuwa na mchakato wa uchaguzi wa amani  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na hadhi inayostahiki kwa kuzingatia katiba ya nchi hiyo kwa minajili ya kuhakikisha utulivu, maendeleo na demokradia katika taifa hilo.

Baraza limesema kuna haja ya kufanya majadiliano ya amani yanayojumuisha pande zote haraka iwezekanavyo ambayo yatajikita katika masuala ya uchaguzi, huku wakihakikisha haki za binadamu na uhuru mwingine unalindwa , lengo ni kufungua njia ya kuhakikisha uchaguzi utakuwa huru, wa haki, wa mani, wenye utulivu, unaojumuisha wote, wa wazi na utakaofanyika kwa wakati nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa kuzingatia katiba huku ukiheshimu misingi ya Afrika ya demokrasia, chaguzi na utawala bora.

Wajumbe hao wa baraza wamesisitiza kwamba wataendelea kuusaidia mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO na mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa.