Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana ndio wenye ufunguo wa mustakhbali wa maendeleo:Ban

Vijana ndio wenye ufunguo wa mustakhbali wa maendeleo:Ban

Vijana ndio walioshika ufunguo wa mustakhbali wa maendeleo katika jamii, lakini mara nyingi hukabiliwa na changamoto katika kujiendeleaza. Kauli hiyo ni kutoka kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa ya ujuzi kwa vijana, akisema zaidi ya vijana milioni 73 kote duniani hawana ajira na kuwafanya kuwa mara tatu zaidi ya watu wazima katika kukosa ajira.

Amesema hususani katika nchi zinazoendelea asilimia kubwa ya vijana hawana ajira rasmi au hifadhi ya jamii, lakini wakiwezeshwa kupitia ujuzi wanaimarisha uwezo wao na kusaidia kushughulikia changamoto zinazoikabili jamii ikiwemo umasikini, kutokuwepo usawa na migogoro.

Naye mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya vijana Ahmad Alhendawi anasema Umoja wa Mataifa kwa kutambua suala hilo unachukua hatua

 (SAUTI AL HENDAWI)

“Nchi wanachama wametoa wito kwa malengo ya maendeleo endelevu kupitisha mkakati wa kimataifa kwa ajili ya ajira kwa vijana, kuitikia wito huo Umoja wa Mataifa umezindua mradi wa kimataifa wa ajira bora kwa vijana, ukijaribu kuzihusisha nchi wanachana, sekta binafsi, jumuiya za vijana na wadau wengine kuwekeza zaidi, kutoa msaada zaidi na kuliweka bayana suala la ajira ya vijana kama kitu muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu”