Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama larefusha vikwazo kwa Ivory Coast

Baraza la Usalama larefusha vikwazo kwa Ivory Coast

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limerefusha muda wa vikwazo kwa Ivory Coast huku pia ikifanyia marekebisho vikwazo vinavyohusu usafirishwaji wa silaha.

Katika azimio lake la pamoja, baraza hilo limekubali kutoa marafuku ya uingizwaji silaha nchini humo lakini kwa zingatio la makundi machache ya watu. Sasa silaha zitaruhusiwa kuingia nchini humo lakini zitakwenda mikononi mwa watu maalumu kama maafisa wa kijeshi wanaotoa mafunzo ya usalama.

Kuhusu kusogezwa mbele kwa vikwazo hivyo baraza hilo sasa limerefusha hadi mwaka 2013 huku pia ikipiga marafuku usafirishwaji wa dhahabu chafu kama inavyojulikana na wengi dhahabu iliyopatikana kwa umwagaji damu.

Ivory Coast ilitumbukia kwenye mkwamo wa kisiasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu uliopita, uchaguzi ulioshuhudia Laurent Gbagbo aking’oka madarakani.