Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS imesikitishwa na kuzuka upya mapigano Sudan Kusini:

UNMISS imesikitishwa na kuzuka upya mapigano Sudan Kusini:

Mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini (UNMISS) umesikitishwa na kuzuka upya kwa mapigano Juba Julai 10 ambayo yanaathiri vibaya raia.

Mapigano makali mjini Juba ikiwa ni pamoja na karibu kaabisa na eneo la UNMISS kwenye nyumba ya Umoja wa mataifa Jebel na Tomping, yamesababisha nwakimbizi wa ndani 1000 kukimbia kutoka eneo la UNMISS la ulinzi wa raia linalowahifadhi (PoC) 1 na kuingia kwenye jingo la UNMISS katika nyumba ya Umoja wa Mataifa ya Jebel.

Pia mapigano hayo katika eneo la viunga vya Juba yamewafungisha virago mamia ya raia na kuwalazimu kusaka usalama kwenye eneo la ulinzi la UNMISS kituo cha Tomping. Umoja wa Mataifa unatiwa hofu na taarifa kwamba majeshi yenye silaha yamezuia raia kukimbia kusaka ulinzi.

Umoja wa mataifa umezitaka pande zote kuheshimu sharia za Umoja wa mataifa na kulaani vikali ulengaji wa makusudi wa maeneo ya Umoja wa mataifa na wafanyakazi wake.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini humo ameutaka uongozi wa Sudan Kusini kuzuia mara moja vikosi vyake , na kujihusisha na mazungumzo kutafuta suluhu ya kisiasa katika mzozo huu na pia kuruhusu Umoja wa Mataifa kuweza kushika doria ili kuwahahakikishia raia usalama.