Kuzijengea nchi uwezo ni muhimu kukabiliana na Tsunami:IOC

21 Juni 2016

Suala la kuzijengea nchi uwezo hasa katika mifumo ya kupasha habari ni muhimu saana katika kukabiliana na kujiandaa na Tsunami. Hayo yamesemwa na Arito Kordia mkuu wa kituo cha Tsunami cha bahari ya Hindi cha shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO (IOC) , kutoka ofisi ya UNESCO Jakarta.

Bwana Kordia yuko Dar es salaam Tanzania kwa ajili ya mradi maalumu unaofadhiliwa na serikali ya Malysia kwa ajili ya mtaifa madogo ya visiwani yanayoendelea na pia ya Afrika yaliyo katika ukanda wa bahari ya Hindi, kuyajengea uwezo wa kuhimi Tsunami mataifa hayo.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayofaidia na mradi huo unaojikita katika kujua athari za Tsunami, jinsi ya kufanya tathimini , kutoa onyo mapema la Tsunami na jinsi ya kukabili hali Tunami ikitokea.

Bwana kodia anasema hayo ni muhimu kwa sababu..

(SAUTI YA KORDIA

“Tsunami na tetemeko huwezi jua lini vinatokea,vinaweza kutokea wakati wowote, na ndio sababu kuwa na uelewa na kujiandaa na pia kujenga uwezo wa maandalizi kama kuna onyo ni lazima viwepo bila kujali lini Tsunami itatokea”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter