Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walemavu wa ngozi sio nyota ya jaha ni binadamu kama wewe: Ikponwosa Ero

Walemavu wa ngozi sio nyota ya jaha ni binadamu kama wewe: Ikponwosa Ero

Watu wenye ulemavu wa ngozi hawawezi kukuletea tija au bahati mbaya, na wala sio nyota ya jaha, ni binadamu wanaotaka kuchukuliwa kama walivyo binadamu wengine.

Huo ni ujumbe wa mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi Ikponwosa Ero, akizungumza mjini Dar es salaam Tanzania katika siku ya pili ya mkutano wa kukabiliana na vitendo vya unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu hao.

Bi Ero ndiye aliyeandaa mkutano huo wa siku tatu na akizungumza na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa mjini Dar es slaam anaelezea yaliyojiri Jumamosi ya leo.

(SAUTI YA ERO)

Ameongeza kuwa leo ilikuwa ni siku ya maneno kidogo vitendo vingi na Umoja wa Mataifa na serikali zimesisitiza umuhimu wa haki za watu wenye ulemavu wa ngozi

(SAUTI ERO 2)