Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustawi wa watu wenye ulemavu waangaziwa

Ustawi wa watu wenye ulemavu waangaziwa

Mkutano wa siku tatu wa nchi wananchama wa mkataba wa kimataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu (CRDPD) umekamilika mjini New York Marekani.

Mkutano huo uliokuwa na maudhui ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030 kwa kujumuisha kundi hili, uliwaleta pamoja wadau wa haki za watu wenye ulemavu wakiwamo wanaharakati wa watu wenye ulemavu lemavu na watu wenye ulemavu.

Barani Afrika ambapo kwa muda mrefu haki na fursa za elimu, afya, taarifa na nyinginezo kwa watu wenye ulemavu zimekandamizwa, wawakilishi wake wamepaza sauti kwa serikali za mataifa yao kuchukua hatua stahiki.Tuungane na Joshua Mmali kwa ufafanuzi zaidi.