Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kutembelea kisiwa cha Lesbos wiki ijayo

Ban kutembelea kisiwa cha Lesbos wiki ijayo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amezungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani baada ya kuhutubia Baraza Kuu juu ya harakati zinazochukuliwa kuimarisha operesheni za ulinzi wa amani.

Mathalani ametaja changamoto za utashi wa kisiasa wa kuchukua hatua pindi wakati watendaji wa Umoja wa Mataifa wanapotekeleza majukumu yao hasa kulinda amani na kuibua ukiukwaji wa haki ..

(Sauti ya Ban)

“Wakati walinda amani wanaposhambuliwa, wanahitaji kuungwa mkono na Baraza la Usalama. Wakati wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanapofukuzwa kwa kutekeleza majukumu yao, wanapaswa kutegemea kuungwa mkono na nchi wanachama.”

Halikadhalika amegusia masuala ya uhamiaji na wakimbizi akizungumzia madhila yanayokumba wasaka hifadhi kutoka maeneo mbali mbali duniani wanaokwenda Ulaya bahari ya mediteranea akisema..

(Sauti ya Ban)

“Nimesikiliza simulizi zao, matarajio na hofu za wakimbizi wengi katika miezi ya hivi karibuni na kuelea changamoto zinazowapata kutokana na uzoefu wao. leo natangaza kuwa nitatembelea kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos, wiki ijayo kutathmini hali ilivyo napia kuonyesha mshikamano.”