Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waanza kuimarisha operesheni za ulinzi wa amani: Ban Ki-moon

Umoja wa Mataifa waanza kuimarisha operesheni za ulinzi wa amani: Ban Ki-moon

Leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaelezea wanachama wa Umoja kuhusu harakati ambazo tayari zinachukuliwa ili kuimarisha operesheni za ulinzi wa amani na ushiriki wa wanawake katika masuala ya usalama. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Lengo la mkutano huo wa Baraza Kuu lilikuwa kuangazia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa baada ya tathmini huru za operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zilizofanyika hivi karibuni.

Bwana Ban amekumbusha kwamba pendekezo la msingi lilikuwa ni kuongeza uwezo wa operesheni hizo kubadilika kutokana na mazingira, na hivyo amesema tayari taratibu za kirasimu zimeanza kurekebishwa.

Kuhusu kesi za uhalifu wa kingono, amesema amechukua hatua thabiti akitegemea pia nchi wanachama kutimiza wajibu wao.

Aidha akasisitiza..

(Sauti ya Ban)

"Acha niwe wazi. Tathmini zimeomba hatua kabambe dhidi ya vitisho hatari. Jibu letu haliwezi kuwa la kawaida. Tunahitaji nchi wanachama kuwajibika, kushikamana na kuwekeza kisiasa na kifedha. Nategemea nchi wanachama kuchukua hatua zaidi ili kuwezesha wanawake na kufanya jamii ziwe na nguvu. "