Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji bunifu wa kilimo unahitajika kupambana na njaa na umasikini:FAO

Uwekezaji bunifu wa kilimo unahitajika kupambana na njaa na umasikini:FAO

Uchagizaji wa kilimo endelevu unahitaji mtazamo mpya utakaojikita katika ubunifu na uwekezaji wa utafiti, teknolojia kwa uwezo wa maendeleo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO José Graziano da Silva kwenye mkutano wa mawaziri wa kilimo wa G-20 uliohitimishwa leo nchini Uchina.

Amesema teknolojia inasaidia katika ufuatiliaji wa ukuaji wa mazao, matumizi ya mbinu mpya , udhibiti wa mashamba na mavuno.

Amesisitiza kwamba teknolojia pia imekuwa nyenzo muhimu katika kuboresha maisha ya watu, kuimarisha masuala ya haki na kuhakikisha fursa sawa hasa maeneo ya vijijini.