Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wengi zaidi wakimbia machafuko Fallujah: UNHCR

Wengi zaidi wakimbia machafuko Fallujah: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema idadi ya watu wanaokimbia machafuko inaongezeka huko Fallujah Iraq, ambapo zaidi ya watu 3000 ikiwa ni kaya zaidi ya 600 wameripotiwa kuhepa eneo hilo.

Idadi hiyo ni ya juma lililopita pekee, kufuatia mashambulizi yakujihami ya vikosi vya Iraq vinavyotaka kuukomboa mji huo.

Shirika hilo linasema zaidi ya wakimbizi 1000 wanaishi katika kambi iliyoko wilayani Fallujah ambapo UNHCR inafanya kazi, huku wengine wakiwa wamesambaa katijka kambi nyingine zinazoendeshwa na serikali.

Shirika hilo limeeleza kuwa vikosi vya Iraq vinasaidi kuwasafirisha watu wanaotaka kukimbia eneo hilo na limeandaa namba maalum ya mawasiliano ili kupata taarifa za raia wanaotaka kukimbia. Pia UNHCR imesema kuwa imepokea taarifa za kujeruhiwa kwa raia mjini Fallujah kutokana na makombora mazito mathalani watu saba wa familia moja walijeruhiwa Mei 28