Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwa hofu na idadi kubwa ya vifo Mediteranea 2016

UNHCR yatiwa hofu na idadi kubwa ya vifo Mediteranea 2016

Mlolongo wa meli kuzama wiki iliyopita kwenye bahari ya Mediteranea , umekatili maisha ya watu 880 limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR) baada ya kuzungumza na manusura.

Mbali ya meli tatu kuzama , boti zingine mbili pia zimezama juma lililopita. UNHCR inasema mwaka 2016 umekuwa ndio wenye vifo vingi , hadi sasa watu zaidi ya 2500 wamepoteza maisha katika miezi mitano ya mwanzo wa mwaka huu ikilinganishwa na zaidi ya 1800 mwaka ja kipindi kama hiki.

UNHCR inajitahidi kuelewa sababu sa maelfu ya watu kuamua kufunga safari hizi zinazohatarisha maisha yao. Nyingi ya boti hizo zinatokea Libya.