Uhuru wa asasi za kiraia bado changmoto: Ban
Uhuru wa asasi za kiraia za kimataifa kufanya kazi bila kuingiliwa uko katika kitisho amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Akiongea katika mkutano kuhusu asasi za kiraia za kimataifa nchini Korea Kusini, Katibu Mkuu amekiri kuwa hata katika Umoja wa Mataifa asasi hizo zimekuwa zikikumbana na vikwazo katika utendaji wake na kutaka hilo lisijirudie.
Ban ametolea mfano namna alivyosikitishwa na hatua ya nchi wanachama kukataa kamati ya kulinda mashauriano ya hadhi ya wanahabari katika tume ya uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa ECOSOC.
Katika hotuba yake wakati wa mkutano wa 66 wa asasi za kiraia (NGOS)za Umoja wa Mataifa chini ya idara mawasiliano ya uma DPI mjini Gyeongju Jamhuri ya Korea, Katibu Mkuu amefafanua mchango wa NGOs) katika kazi ya Umoja wa Mataifa na nguvu ya asasi hizo katika mustakabali sawia .