Mwelekeo ni vifungashio vya sigara bila alama yoyote- WHO

31 Mei 2016

Ujumbe wetu wa mwaka huu wa siku ya kutotumia bidhaa za tumbaku unalenga vifungashio vya sigara visivyokuwa na alama wa jina kama njia ya kupunguza matumizi ya bidhaa hizo, amesema Dkt. Ahmed Ouma, Mshauri wa masuala ya tumbaku katika ofisi za WHO kanda ya Afrika.

Akihojiwa na idhaa hii, Dkt. Ouma amesema....

(Sauti ya Dkt. Ouma)

Amesema pamoja na vifungashio visivyo na alama wala picha WHO inataka nchi wanachama..

(Sauti Dkt. Ouma)

Hadi sasa ni nchi sita tu Afrika ambazo zimekidhi hatua ya kuweka onyo la kiafya na picha na nchi hizo ni Chad, Burkina Faso, Seychelles, Mauritius, Madagascar na Namibia.

Halikadhalika Dkt. Ouma amezungmzia hali ya matumizi ya uvutaji sigara barani Afrika akisema inatia wasiwasi mkubwa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 15 ambapo mmoja kati ya vijana watano anatumia bidhaa za tumbaku na hivyo kutaka serikali ziimarishe kampeni dhidi ya matumizi ya tumbaku.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter