Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yatata nchi kuheshimu makubalino ya WTO yanayozingatia upatikanaji wa dawa bila vikwazo

UNAIDS yatata nchi kuheshimu makubalino ya WTO yanayozingatia upatikanaji wa dawa bila vikwazo

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na UKIMWI UNAIDS limetaka kuwepo kwa umakini kuhakikisha kwamba matakwa ya kibiashara yanayofungwa baina ya mataifa hayawi kizingiti kwa baadhi ya nchi kushindwa kufikiwa na madawa ya HIV.

Shirika hilo limesema kuwa kiu ya kibiashara isivuke mipaka na kushindwa kutambua makubalino yaliyofikiwa na shirika la biashara ulimwenguni WTO ambayo inasisitiza kuwepo kwa fursa ya kila nchi kufikiwa na madawa ya HIV.

 

UNAIDS katika taarifa yake imeeleza kuwa inaunga mkono makubaliano ya Dowa yanayotilia msukumo kuwepo kwa fursa isiyo na vikwazo kwa nchi kupata huduma ya madawa hayo ya kukabiliana na UKIMWI.

 

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika hilo, inakadiriwa kuwa watu zaidi ya milioni 33 dunaini kote wameambukizwa virusi vya HIV.