Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumbuizo katika mkutano wa utu wa kibinadamu #WHS

Tumbuizo katika mkutano wa utu wa kibinadamu #WHS

"Mtazamo wa uhamiaji na wahamiaji unachukuliwa kama kitu kibaya". Hiyo ni kauli ya mkurugenzi mkuu wa Shirika la uahamiaji duniani IOM William Swing alipohutubia mkutano wa utu wa kibindamu uliofanyika Mei 23 hadi 24 mjini Istanbul Uturuki. Bw. Swing anasema kwamba ni lazima mtazamo huo ubadilidhwe ikizingatiwa kwamba nchi nyingi zimejengwa kwa nguvu za wahamiaji na kwamba uhamiaji ni kitu kizuri na ni vyema kurejelea dhana hiyo. Hayo ni miongoni ya mambo yaliyofanyika katika mkutano huo wa kwanza wa aina yake, ulioambatana pia na burudani murua kama anavyosimulia Grace Kaneiya katika makala hii.