Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa #WHS uwe na matokeo- Eliasson

Mkutano wa #WHS uwe na matokeo- Eliasson

Mkutano wa dunia kuhusu utu wa kibinadamu ukitarajiwa kuanza kesho huko Istanbul, Uturuki, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ametaka utu wa kibinadamu kupatiwa kipaumbele kwenye mkutano huo wa siku mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bwana Eliasson ametaja mambo matano ambayo yanapaswa kuwa msingi wa majadiliano, ikiwemo kuzuia mizozo, kuzingatia sheria za kibinadamu na kuwekeza katika kazi za usaidizi wa kibinadamu.

Bwana Eliasson amesema matarajio ni ahadi za serikali ambazo zitabadilishwa kuwa vitendo na kwamba..

(Sauti ya Eliasson)

“Tunaweka mwelekeo, lakini nafahamu tunafahamu kuwa mnafahamu ili kufikia lengo hilo ni lazima tufanye kazi kwa bidi na tuchukue kama siyo mamia ya hatua basi maelfu. Lakini jambo zuri la kuwa na matarajio au mpango kama tulio nao sasa ni kuwa tunafahamu mwelekeo wa kwenda.”

Zaidi ya watu 6000 wakiwemo wakuu wa nchi, wafanyakazi wa kibinadamu na wawakilishi wa mashirika ya kiraia na jamii zilizoathirika, wanatarajiwa kushiriki mkutano huo wakijadili jinsi ya utoaji misaada ya kibinadamu unaweza kufikia wahitaji wengi zaidi.