Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia 50,000 hatarini kutumiwa kama ngao vitani Fallujah- UNHC

Raia 50,000 hatarini kutumiwa kama ngao vitani Fallujah- UNHC

Takriban raia 50,000 walionaswa katika mji wa Fallujah nchini Iraq, wamo katika hatari ya kutumiwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh kama ‘ngao’ katika mapigano, kwa mujibu wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini humo, Lise Grande.

Vikosi vya muungano vinavyoongozwa na serikali ya Iraq, vilianza mashambulizi dhidi ya Daesh au ISIL mnamo Jumapili wili iliyopita, kwa lengo la kuukomboa mji wa Fallujah, ambao umekuwa chini ya kikundi hicho chenye itikadi kali katili, tangu Januari mwaka 2014.

Bi Grande amesema mashirika ya Umoja wa Mataifa yanafanya kila yawezalo kuwalinda raia hao. Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa, ameeleza kuhusu hali ya kibinadamu ya sas.

(Sauti ya Grande)

“Kimsingi ni miezi minne na nusu sasa au mitano sasa tangu wamepata mgao wa kawaida wa chakula pamoja na dawa. Na zaidi ya hayo sasa ni mashambulizi ya kijeshi.”

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR na mdau wake, Muslim Aid, yamekuwa yakitoa misaada ya dharura kwa watu walioweza kukimbia kutoka Fallujah, na yatafungua kambi mpya karibu na Fallujah wiki ijayo.