Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwepo wa wanawake katika ulinzi wa amani haukwepeki: Ladsous

Uwepo wa wanawake katika ulinzi wa amani haukwepeki: Ladsous

Ushirikishwaji wa wanawake katika katika ulinzi wa amani umeleta mabadiliko yanayoshawishi umuhimu wa jukumu hilo, amesema Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa, Herves Ladsous. Taarifa zaidi na Joshua Mmali

(TAARIFA YA JOSHUA)

Akizungumza katika mahojiano maalum na redio ya Umoja wa Mataifa kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa Mei 29, Ladsous amesema tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Uslama kuhusu wanawake, amani na usalama, uhusiano wa moja kwa moja kati ya kundi hilo na amani umeongezeka.

Amesema hilo limesababisha maendeleo kwani.

(SAUTI LADSOUS)

‘‘Tuna kati ya asilimia 11 hadi 12 ya wanawake katika kikosi cha polisi wa Umoja wa Mataifa na tumeunda vikosi kadhaa vya polisi wanawake pekee ili kushugulikia masuala maalum ya wanawake katika nchi.’’

Elizabeth Kavira ni miongoni mwa raia waliohudumiwa na kikosi cha kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, MONUSCO kilichokitowesha waasi wa M23.

( SAUTI ELIZABETH)