Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania imepiga hatua huduma za afya na elimu, bado changamoto- Ripoti

Tanzania imepiga hatua huduma za afya na elimu, bado changamoto- Ripoti

Tanzania imepata maendeleo ya kuridhisha katika utoaji huduma za elimu na afya, hususan miundombinu ya afya vijijini na mahudhurio ya walimu.Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya viashiria vya utoaji huduma iliyotolewa hii leo jijini Dar es salaam.

Hata hivyo ripoti hiyo inaweka mambo yanayosababisha kiwango kidogo cha uelewa kwenye elimu ya msingi ambapo mtoto mmoja kati ya wanne walio darasa la nne hawezi kusoma aya ya Kiswahili.

Keith Hansen, Makamu Rais wa Benki ya Dunia idara ya uendelezaji rasilimali watu.

 (Sauti Keith)

“Watoto wengi wako shuleni lakini hawajifunzi stadi za msingi za lugha na hisabati kama tulivyoona katika baadhi ya takwimu hizi. Vifo vya watoto wachanga na wajawazito bado ni changamoto kubwa kupunguza. Ni wazi kufanya kazi kwa mazoea hakuwezi kuendelea. Kwa sasa Tanzania inarekebisha mifumo yake ili iweze kupata matokeo bora kwa changamoto inazokabili ”

Bwana Keith amesema Benki ya Dunia inajivunia kushirikiana na Tanzania ili kufanikisha malengo yake ya kuendeleza rasilimali watu na kupunguza umaskini.