Skip to main content

Miji ina jukumu katika uhamiaji:Clos

Miji ina jukumu katika uhamiaji:Clos

Miji hususani barani Ulaya ina jukumu la kibinadamu kukubali wahamiaji amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la makazi Joan Clos.

Mwaka jana wahamiaji na wakimbizi milioni moja na nusu waliwasili Ulaya wengi wao wakiwa na matumiani ya kujenga upya maisha yao katika maeneo ya mijini.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa Bwana Clos anasema kwanini uhamiaji ni suala la miji.

(Sauti ya Clos)

‘Kwasababu ya misukumo ya kiuchumi kwa miji, watu wanasaka maisha bora na pia sababu nyingine kwamba kukiwa na machafuko watu hutaka kujilinda. Miji ni sehemu ambayo hatimaye uhamiaji hufanyika.’’

Kadhalika ameelezea jukumu na UN Habitat katika kuhakikisha uhamiaji mijini unatekelezeka.

(Sauti ya Clos)

‘‘Mara zote tunajaribu kufafanua kile kinachoendelea duniani, ili kwamba serikali za ngazi zote, kitaifa na kikanda na za mitaa zijue kinacheondelea duniani.”