Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 10 ya mkutano wa ujasiriamali na ubunifu wa UNCTAD

Miaka 10 ya mkutano wa ujasiriamali na ubunifu wa UNCTAD

Leo ni miaka kumi tangu kufanyika kwa mkutano wa viongozi kuhusu ubunifu na ujasiriamali ulioandaliwa na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD ambapo jijini New York, Marekani kumeanza mkutano aw siku mbili kutathmini tukio hilo.

Mkutano huo umekutanisha watendaji kutoka taasisi mbali mbali zinazojinasibu kwa ubunifu na ujasiriamali kwa lengo la kuboresha maisha ya wakazi wa sayari ya dunia kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Miongoni mwao ni Frank Drohan, mwenyekiti wa kampuni ya Imagine inayohusika na miradi kwa maslahi ya kufanikisha SDGs ambaye amesema ramani ya utekelezaji wa malengo hayo ina takwimu za aina yake hivyo akatoa wito kwa wajasiriamali na wabunifu kwenye mkutano huo..

(Sauti ya Frank)

“Fuata ramani hiyo, itumieni kuandaa bidhaa zenu, miradi na hata taasisi zenu, na matokeo yake mtapata faida, mtakuwa bora zaidi kwa kufanya jambo jema. Hii ni njia ya kuangalia biashara kwa jicho ambalo si la kibiashara. Ni jambo la hekima sana.”