Ukosefu wa ajira nzuri unatishia kupunguza umasikini imeonya ILO

Ukosefu wa ajira nzuri unatishia kupunguza umasikini imeonya ILO

Miongo ya hatua zilizopigwa katika kupunguza umasikini inaweza kuenguliwa na ukosefu wa ajira zenye hadhi na kudumaa kwa uchumi wameonya leo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya ajira.

Kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO , theluthi ya wafanyakazi katika nchi masikini wanapata chini ya dola dola 3.10 kwa siku.

Mkuu wa ILO Guy Ryder ameonya dhidi ya ongezeko la kutokuwepo usawa wa kipato na matarajio mabaya kwa mataifa ya Asia, Amerika ya Kusini na Kanda ya nchi za Kiarabu kunatishia lengo la maendeleo endelevu la kukomesha umasikini ifikapo 2013.

Ameongeza kuwa kutokuwepo kwa usawa katika mshahara kunaendelea kuathiri Ulaya.

Ili kutokomeza umasikini ifikapo 2030 ripoti ya mtazamo wa ajira duniani 2016 inatoa wito wa kuwa na kazi bora zaidi na zenye uzajishaji. Na ili kufanikisha hili Bwana Ryder anasema nchi zinapaswa kuweka mtazamo wa kuwaingiza wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi katika sekta rasmi hali ambayo itawasaidia wafanyakazi kufaidika na ulinzi wanaostahili katika jamii.

(SAUTI YA GUY RYDER)

Hii ni ajenda ambayo serikali za Afrika , wafanyakazi, vyama vya wafanyakazi, wanahitaji kuwa sehemu ya ajenda hiyo, sawa na mataifa ya Amerika Kusini na Asia. Hivyo nadhani kuna matumizi halisi ya kitaifa ya ajenda hii ya kurasimisha na dhamira ya kweli ya kisiasa ya kusonga kwenda mbele ... hii ni muhimu katika kufuta umaskini kazini. "