Skip to main content

UNAMI yalaani vikali shambulio mjini Sadr na Baquba Iraq

UNAMI yalaani vikali shambulio mjini Sadr na Baquba Iraq

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq , Ján Kubiš, amelaani vikali shambulio la bomu la kutengwa kwenye gari lililotokea leo kwenye moja ya soko lililo na shughuli na watu wengi mjini Sadr na kukatili maisha ya watu wengi na kujeruhi lukuki.

Shambulio hilo limekuja baada bomu lingine kulipuka kwenye gari karibu na mgahawa mjini Baquba Mei 9 na kusababisha vifo na majeruhi wengi.

Mashambulio hayo ni vitendo vya uoga vya kigaidi dhidi ya raia wasio na hatia bali waliokuwa wakiendelea na maisha yao kama kawaida amesema Bwana Kubiš na kuongeza kuwa vitendo hivyo ni kinyume na misingi ya utu na ubinadamu na nilazima vilaaniwe vikali..