UM walaani washambulio kinyume cha sheria Syria

UM walaani washambulio kinyume cha sheria Syria

Tume Huru ya Kimataifa ya uchunguzi kuhusu Syria imelaani vikali mashambulio ya hivi karibuni dhidi ya raia na miundombinu ya umma kama hospitali na kliniki katika mji wa Aleppo, na pia dhidi ya wakimbizi wa ndani katika kambi ya Idlib. John Kibego na taarifa kamili.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Tume hiyo imezitaka pande zinazozozana kusitisha mashambulio kinyume cha sheria, dhidi ya makaazi ya raia hasa katika maeneo maalum ya kibinadamu na yale yanayopaswa kulindwa chini ya sheria ya kimataifa.

Imefuatia mashambulio ya angani na uvurumishwaji wa mizinga na roketi ambavyo vimetumiwa sana hivi karibuni, kutekeleza mashambilio ya kiholela dhidi ya maeeno yanayohifadhi raia walio hatarini.

Watu kadhaa waliripotiwa kuuwawa au kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani ya Idlib mnamo Mei, tano.

Tangu mashambulio dhidi ya hospitali ya Al-Quds mjini Aleppo April 27, zaidi ya mashambulio sita yameshuhudiwa kwenye vituo vya afya yakisababisha vifo au majeraha kwa raia na wauguzi kadhaa, huku uharibifu wa chakula, maji na vifaa tiba vikitishia uhai wa wanachi katika mji wa Aleppo.