Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awasili Mauritius na kukutana na Rais wan chi hiyo:

Ban awasili Mauritius na kukutana na Rais wan chi hiyo:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili Jumapili katika Jamhuri ya Mauritius na kukutana na Rais wan chi hiyo Dr. Ameenah Gurib-Fakim.

Viongozi hao wawili wamejadili utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na hususani hali ya mataifa yanayoendelea nya visiwa vidogo SIDS.

Katibu Mkuu amepongeza uongozi na mafanikio ya taifa hilo mada hizo. Ban na Rais Gurib-Fakim pia wamebadilishana mawazo kuhusu ushiriki wa Mauritius kwenye kongamano la ngazi ya juu la kisiasa mwaka 2016.

Katibu Mkuu pia amemshukuru Rais huyo kwa kukubali mwaliko wa kuwa mwenyekiti mwenza kwenye mjadala wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa na Bank ya dunia kuhusu maji.