Ban alipongeza bunge la Ushelisheli kwa demokrasia na nafasi za wanawake:
Juhudi zilizofanya kwa Kisiwa cha Ushelisheli katika kufikia malengo ya maendeleo yaani MDG’s ni ishara kwamba inawezekana kuendelea kiuchumi, huku huduma za afya, elimu, kuwajali wasiojiweza na kulinda mazingira vikiwezekana.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu aqwa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia bunge la Ushe;isheli leo Jumapili na kulipongeza kwa rekodi nzuri katika demokrasia akitolea mfano hatua ya karibuni ya kupitisha sharia ya kuwa na muhula maalumu wa Urais.
Pia amelitaka bunge hilo kuendeleza jitihada za kuongeza nafasi za wanawake na kufikia asilimia 50-50. Amelisa bunge hilo kuwashirikisha vijana kwa sababu
(SAUTI YA BAN)
“Umoja wa Mataifa unawaona vijana sio kama viongozi wa kesho bali viongozi wa leo. Tunafanya kazi na wavulana na wasichana kote duniani katika miradi ya ujenzi wa Amani, kuunda nafasi za kazi na kupambana na ghasia zitokanazo na itikadi kali”
Ameitaka Ushelisheli kuona mbali Zaidi y a kisiwa hicho na kuwa raia wa kimataifa katika kushiriki kupata suluhu ya changamoto zinazoikabili dunia.
