Kongamano la WSIS 2016: kuimarisha nguvu ya teknolojia mpya kuendesha maendeleo

3 Mei 2016

Wajumbe wa kimataifa takribani 1800 wakiwemo wadai wa serikali, asasi za kiraia na wataalamu wa teknolojia wanakutana Geneva, Uswisi wiki hii kuunda mikakati ya kimataifa ya kufikia malengo ya uunganishwaji na teknolojia yaliyowekwa Tunis, Tunisia.

Wajumbe hao wanakutana kwenye mkutano wa Umoja wa mataifa wa dunia kuhusu mfumo wa habari na mawasiliano (WSIS) kwa lengo moja tuu, la kuibadili dunia kupitia uwezo wa teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuchagiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenda sanjari na utumizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.

Akizungumza kwenye kongamano hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa amewaasa washiriki kuahakikisha khakuna anayesalia nyuma katika teknolojia ya mawasiliano.

(SAUTI YA BAN)

"Ninawahimiza nyote kuendelea kufanya kazi ya kuhakikisha kila mtu anapata teknologia ya mawasililano. Hebu tuwezeshe watu wote kila pahala na teknolojia hii mabadiliko ili nao wasaidie katika ujenzi wa maisha bora kwa wote…"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud