Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apokea mwenge wa Olympiki

Ban apokea mwenge wa Olympiki

Miezi mitatu kabla ya michuano ya Olympiki nchini Brazil, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepokea mwenge wa Olympic katika ofisi za Umoja huo mjini Geneva uliobebwa na mtoto mwenye umri wa miaka 13, kutoka nchi mwenyeji wa michuno hiyo Brazil.

Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya michezo kwa maendeleo Katibu Mkuu amekaribisha uamuzi wa waandaji wa michuano hiyo wa kujumuisha timu ya wakimbizi kwa mara ya kwanza.

Ban amesema hiyo haitoshi na hivyo.

(SAUTI BAN)

‘‘Naitaka dunia kutafuta suluhisho la kudumu. Wakimbizi wanahitaji makazi sio mahema. Wanataka bendera inayotetea haki zao. N wanastahili dunia inayowapa zaidi ya msaada, dunia yenye amani. Wote tuiunge mkono timu ya wakimbizi hadi pale kutakapokwua hakuna haja ya timu ya wakimbizi.’’