Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Silaha za kemikali zimeibuka tena vitani- Ban

Silaha za kemikali zimeibuka tena vitani- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema matumizi ya silaha za kemikali yameibuka tena katika vita.

Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya kumbukizi ya wahanga wa vita vya kemikali, ambayo huadhimishwa kila mwaka Aprili 29.

Ameongeza kwamba badala ya kusalia katika vitabu vya historia, matumizi ya silaha za kemikali yameibuka tena.

Bwana Ban amesema kwamba dunia imeshuhudia ushahidi mpya wenye kutia majonzi wa mateso ya wahanga wa silaha hizo, kwa mfano kwenye mzozo wa Syria.

Mkataba wa kupiga marufuku silaha za kemikali ulioridhiwa mwaka 1992, unatoa wito wa usitishwaji wa silaha za kemikali ambapo kwa sasa nchi 192 zimeridhia mkataba huo.

Umoja wa Mataifa unasema kwamba uharibifu wa viwanda vya kutengeneza silaha za kemikali umepanda hadi asilimia 90.