Skip to main content

Watu milioni 2 hufa kila mwaka kutokana na hatari na magonjwa kazini:UM

Watu milioni 2 hufa kila mwaka kutokana na hatari na magonjwa kazini:UM

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya usalama na afya kazini, mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu na vitu vya madhara na taka, Baskut Tuncak, amezitaka nchi na kampuni za biashara kuongeza juhudi za kuzuia vifo na magonjwa yatokanayo na vifaa vyenye madhara kazini.

Amesema kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO, takriban watu milioni mbili hufa kila mwaka kutokana na maradhi yanayoambatana na kazi. Na maradhi mengi kama saratani, ugonjwa wa mapafu, maradhi ya moyo , mimba kuharibika, kujifungua watoto wenye ulemavu na athari zingine za kiafya ni matokeo ya athari za kemikali zenye madhara.

Wafanyakazi ni miongoni mwa kundi lililo katika hatari ameonya mtaalamu huyo katika ujumbe maalumu wa siku hii ya kimataifa ya usalama na afya kazini ambayo pia hujulikana kama siku ya kimataifa ya kuwaenzi wafanyakazi waliokufa na kujeruihiwa. Kila mwaka huadhimishwa Aprili 28.

Ameongeza kuwa kuzuia na kuchukua tahadhari lazima viwe katika kipaumbele kwenye juhudi za nchi na biashara ili kulinda haki za wafanyakazi