Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakutana kuhusu uharamia Ghuba ya Guinea

Baraza la Usalama lakutana kuhusu uharamia Ghuba ya Guinea

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekuwa na mjadala wa wazi leo kuhusu uharamia na wizi wa kutumia silaha katika Ghuba ya Guinea, kulingana na ajenda ya kuimarisha amani Afrika ya Magharibi.

Katika taarifa ya Rais wake, Baraza hilo limelaani vikali vitendo vya mauaji, utekaji nyara, na wizi unaofanywa na maharamia katika Ghuba ya Guinea.

Aidha, wajumbe wa Baraza hilo wameeleza kutiwa wasiwasi na visa vingi vya uhalifu huo, na kiwango cha ukatili unaotokana na vitendo vya uharamia na wizi wa kutumia silaha baharini, ambavyo vimeripotiwa tangu mwaka 2014.

Halikadhalika, Baraza la Usalama limekariri kuwa kukabiliana na tishio la uharamia na wizi wa kutumia silaha na vyanzo vyake katika Ghuba ya Guinea, ni jukumu la msingi la serikali za ukanda huo, kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kwenye ukanda huo na wadau wengine.