Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo ni kiwango cha chini tunachohitaji:Nabarro

Ajenda ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo ni kiwango cha chini tunachohitaji:Nabarro

Malengo ambayo serikali zimejiwekea katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu ni ya kiwango cha chini ambacho dunia inahitaji.

Huo ni mtazamo wa mshauri maalumu kuhusu ajenda ya mwaka 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi, David Nabarro  akizungumza kabla ya  hafla maalumu ya ngazi za juu itakayofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York siku ya Ijumaa ya utiaji saini mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi uliopitishwa Paris mwaka jana.

 (SAUTI YA NABARRO)

‘‘Malengo 17 ya maendeleo endelevu yanagusa maendeleo muhimu kwa watu ambayo ni muhimu kwa mustakabali endelevu, na lengo namba 13 linahusiana na mabadiliko ya tabia nchi.’’