Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za pamoja zinahitajika kutimiza SDGS: Eliasson

Juhudi za pamoja zinahitajika kutimiza SDGS: Eliasson

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa ngazi ya juu kuhusu kufanikisha melengo ya maendeleo endelevu SDGS, sambamba na fursa ya makataba wa mabadiliko ya tabianchi COP21 katika kutekeleza ajenda ya 2030. Taarifa zaidi na Amina Hassan..

(TAARIFA YA AMINA)

Nuts...

Hii ni filamu iliyoshuhudiwa na hadhira hii ambayo imeonyesha mustakabali wa dunia katika kutekeleza ajenda ya 2030 .

Akihutubia katika mjadala huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema kuelekea mwaka mmoja tangu wakuu wa nchi kusaini malengo hayo mwezi Septemba mwaka jana, anataja kile kinachohitajika kutimiza SDGS...

( SAUTI JAN)

‘‘Jitihada za pamoja kutoka kwa serikali zote, na wadau wengine. Tunahitaji kutumia mbinu jumuishi katiaka jitihada za maendeleo kwa kuwaunganisha wadau wa misaada ya kibinadamu na hakiza binadamu, jamii zenye amani na taasisi hai.’’

Wawakilishi wa vijana barubaru ni miongoni mwa wawasilishaji wa mada waliozungumzia hatma yao kupitia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGS.