Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya Somalia azuru AU

Mtaalamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya Somalia azuru AU

Mtaalamu huru kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Somalia Bwana, Bahame Tom Nyanduga amemtembelea mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika kwa ajili ya Somalia (SRCC) , Balozi Francisco Madeira mjini Moghadishu.

Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo hatua iliyochukuliwa na mpango wa muungano wa Afrika wa kulkinda Amani Somali AMISOM , wa kuhakikisha mpango huo unatekeleza sharia za kimataifa za masuala ya kibinadamu na kuheshimu haki za binadamu katika operesheni zake za kulinda Amani Somalia.

Bwana Nyanduga ameipongeza AMISOM kwa jukumu lake la kurejesha usalama Somalia na luitaka kuhakikisha inatimiza wajibu wake wa kimataifa kwa kuzingatia sharia na haki za binadamu katika sera zake..

(SAUTI YA NYANFUGA)