MJUMITA na mbinu mbadala ya uchomaji mkaa

MJUMITA na mbinu mbadala ya uchomaji mkaa

Wakati kesho zaidi ya nchi 130 zikitarajiwa kutia saini mkataba wa mabadiliko ya tabianchi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu, MJUMITA umetaja mafanikio ambayo yamepatikana katika kuelimisha wananchi kuhusu uhifadhi wa misitu.

Akihojiwa na idhaa hii, Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA Rahima Njaidi ametaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na uvunaji endelevu wa misitu kwa ajili ya kuchoma mkaa akisema..

(Sauti ya Rahima-1)

Rahima akaeleza mafanikio ambayo wamepata katika uhifadhi misitu kwenye mikoa 13 na vijiji 452 ambako MJUMITA inaendesha shughuli zake za kusaidia wananchi kuhifadhi misitu inayowazunguka.

(Sauti ya Rahima-2)