Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa asili na utiaji saini mkataba wa Paris

Watu wa asili na utiaji saini mkataba wa Paris

Hindou Oumarou Ibrahim, mwanamke kutoka jamii ya watu wa asili kutoka Mbororo jamii ya wafugaji nchini Chad ni miongoni mwa wazungumzaji waliochaguliwa kuwakilisha asasi za kiraia kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa kihistoria wa mabadiliko ya tabianchi siku ya Ijumaa. Assumpta Massoi namaeleo kamili.

(TAARIFA ASSUMPTA)

Idadi kubwa za nchi zinatarajiwa kutia saini mkataba huo katika hafla iliyoandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Aprili 22 ambayo pia ni siku ya kimataifa ya “Dunia Mama”.

Kwa mujibu wa Bi Ibrahim ambaye ni mratibu wa shirika la kijamii la (AFPAT) linalohusika na hali na ulinzi wa mazingira kwa wanawake watu wa asili wa Peule na watu wa Chad,kwa watu wote wa asili kila kona ya dunia maisha yao yanahusiana na mali asili kwa ajili ya chakula, dawa,na kila kitu hivyo kukiwa na mafuriko au ukame athari zake ni kubwa sana kwa jamii za watu wa wa asili.

Ameongeza kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanatishia haki za msingi za watu wa asili, utamaduni wao na mustakhbali za jamii hizo. Bi Ibrahim mwenye umri wa miaka 32 amekulia jamii ya wafugaji na hivyo anatambua changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kwa jamii za watu wa asili.