Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zote Yemen zimuunge mkono mwakilishi maalumu:Ban

Pande zote Yemen zimuunge mkono mwakilishi maalumu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amezitaka pande zote katika mchakato wa amani nchini Yemen kushirikiana kwa moyo mkunjufu na mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed, ili majadiliano ya amani yaanze bila kuchelewa zaidi

Katibu Mkuu amerejea wito wake wa wajibu wa kila upande katika kusitisha uhasama ambao ulianza rasmi April 10, na pia katika kuitishwa kwa mazungumzo ya amani ya Yemen huko Kuwait April 18.

Amesema anatambua kwamba ujumbe wa serikali ya Yemen umewasili Kuwait na unatazamia ushiriki wa Ansar Allah na wawakilishi wa General People’s Congress (GPC) .

Ban amesema anshawishika kwamba kutumia fursa hii kusongesha mbele mchakato kutasaidia kutatua masuala kadhaa na kukomesha machafuko ya muda mrefu, kwani watu wa Yemen na ukanda mzima wamechoshwa na vita.