Uhaba wa maji Tanzania na harakati za kukwamua
Maji, maji, maji! Hiki ni kilio cha wengi hususani barani Afrika. Leo dunia ikiadhimisha siku ya maji, nchini Tanzania upatikanaji wa maji ni changamoto kubwa hususani katika baadhi ya maeneo mkoani Kagera. Baadhi ya vijana kwao ni fursa ya kujipatia kipato. Kulikoni? Ungana na Tumaini Anatory wa redio washirika Karagwe Fm ya Kagera Tanzania katika makala itakayokupa undani kuhusu kadhia hiyo ya upatikanaji wa maji.