Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Washindi wa shindano la michoro watangazwa

Washindi wa shindano la michoro watangazwa

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imetangaza washindi wawili wa shindano la bango kwa watoto la kuelezea uhuru una maana gani kwao, shindano ambalo liliendeshwa kwa vigezo vya umri.

Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya mikataba miwili ya kimataifa ule wa uchumi, kijamii na utamaduni na mkataba wa haki za kiraia na kisiasa ambapo mshindi katika kundi la miaka mitano hadi 11 ni Alexandria Slaven kutoka Samoa mweneyumri wa maiaka 11, aliyechora ya watu walioshikana mikono wakiwa wamesimama chini ya mti wa mnazi.

Mshindi katika kundi la umri wa miaka 12 hadi 18 ni Eiza Abid, mtoto mwenye umri wa miaka 15 kutoka Pakistan. Mtoto huyu kwa kutumia rangi nyeusi na nga’avu ameonyesha uhuru wa mawazo.

Ubunifu wa watoto hao ambao utawekwa katika mabango na kutumika katika kampeni, ulichaguliwa katika washindi wa mashindano ya Umoja wa Mataifa yaliyoandaliwa katika nchi saba zikiwamo Burundi, Armenia, Fiji, Madagascar, Pakistan, Samoa na Tunisia.

Washindi katika mashidnao hayo na maelezo yanapatikana kwa kubofya katika mtandao wenye tovuti ya kampeni.