Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado hakuna usawa kijinsia kazini: ILO

Bado hakuna usawa kijinsia kazini: ILO

Shirika la Kazi Duniani ILO limezindua leo ripoti yake kuhusu wanawake kazini, ikionyesha kwamba licha ya mafanikio katika elimu ya wanawake, bado tofauti kati ya wanaume na wanawake kazini hazijapungua.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva Uswisi, Naibu Mkurugenzi wa idara ya Utafiti wa ILO Lawrence J. Johnson amesema kwamba wanawake zaidi wanakosa ajira bora na hata ajira kabisa. Ameongeza kwamba takwimu zinaonyesha kuwa wanawake wanafanya kazi za nyumbani mara 2 hadi mara tatu zaidi kuliko wanaume, ikipunguza uwezo wao wa kuwa na kazi yenye mshahara.

Na kuhusu tofauti za mishahara amesema

(Sauti ya Bwana Johnson)

“ Wanawake wanapata kipato kidogo kuliko wenzao wa kiume. Tofauti ya mshahara inakadiriwa kuwa asilimia 23. Licha ya mabadiliko madogo katika pupunguza tofauti za mishahara, inakadilriwa kuwa itachukua zaidi ya miaka sabini kutimiza usawa huo ikiwa hali itasalia kuwa ilivyo sasa.”