Ufadhili mpya wasaidia WFP kutimiza mahitaji ya Wasyria

Ufadhili mpya wasaidia WFP kutimiza mahitaji ya Wasyria

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP limepata ufadhili wa kutosha wa kurejesha misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Syria waliopo Jordan, Lebanon, Iraq na Misri hadi mwisho wa mwaka.

Taarifa iliyotolewa leo imeeleza kwamba usaidizi huo umepatikana kupitia ufadhili mpya ulioahidiwa wakati wa kongamano la kimataifaku husu mahitaji ya kibinadamu Syria uliofanyika mjini London Uingereza hivi karibuni. WFP imesema dola milioni 675 zimeahidiwa, miongoni mwao milioni 623 zikiwa zimetolewa na Ujerumani.

Kwa sasa ni wakimbizi wa Syria milioni 1.8 na watu wengine milioni 4.5 ndani ya nchi ambao wanategemea usaidizi wa WFP kwa chakula kila siku.