Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mada mbalimbali likiwemo suala la Wapalestina zapewa uzito kwenye Baraza Kuu

Mada mbalimbali likiwemo suala la Wapalestina zapewa uzito kwenye Baraza Kuu

Kikao cha Baraza Kuu cha 66 kimeanza wiki hii kwenye Umoja wa Mataifa hapa New York.

Mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo maradhi yasiyo ya kuambukiza yaani NCD’s, masuala ya nyuklia, hali ya Libya, kutokomeza jangwa na ijumaa hii suala la Palestina kutaka kuwa taifa huru na kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema umefika wakati watu wa Palestina wakaishi kwa uhuru, amani na matumaini kama binadamu wengine baada ya kuwasilisha rasmi ombi la uanachama kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Lakini waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amani ya Mashariki ya Kati itapatikana tu kwa Israel na Palestina kuketi pamoja kujadili mustakhbali wao, na tatizo sio makazi ya Walowezi bali ni matokeo ya kushindwa kufikia muafaka wa amani.

Nchi mbalimbali zimekuwa na msimamo wake kuhusu suala hili la Palestina. Mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Kenya Moses Wetangula kuhusu baadhi ya mada zilizojadiliwa ikiwemo suala la Wapalestina. Wasikilize

(MAHOJIANO YA FLORA NA WETANGULA))