Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP imekuwa sambamba na Kenya katika kuondoa umaskini

UNDP imekuwa sambamba na Kenya katika kuondoa umaskini

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP likitimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, Kenya imesema chombo hicho kimekuwa  mstari wa mbele katika kusaidia kuondoa umaskini tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1963.

Akihojiwa na idhaa hii jijini New York, Marekani kando ya mkutano wa ngazi ya mawaziri katika kuadhimisha siku hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya mipango nchini Kenya Saitoti Torome amesema UNDP imesaidia tafiti za hali ya umaskini ambazo zimewezesha kuelekeza fedha maeneo yenye uhitaji zaidi akitaja fedha za mfuko wa maendeleo jimboni, CDF..

(Sauti ya Saitoti)

Bwana Saitoti akasema sambamba na hilo amewaeleza washiriki utekelezaji wa awamu ya pili ya dira ya maendeleo 2030 ya Kenya, MTP TWO ikiwemo ..

(Sauti ya Saitoti)