Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yahaha kusaidia watoto waliokumbwa na unyafuzi Malawi

UNICEF yahaha kusaidia watoto waliokumbwa na unyafuzi Malawi

Ukame uliopitiliza nchini Malawi umesababisha njaa iliyokithiri. Watoto ndio wameathirika zaidi kwani hawapati lishe bora na kutishia uhai wao. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema kiwango cha utapiamlo uliokithiri au unyafuzi kimeongezeka kwa asilimia 100 kati ya Disemba 2015 na Januari 2016.  Bei za vyakula zimepanda, shughuli za kiuchumi ikiwemo biashara za mazao zimeporomoka. Serikali imeomba msaada ili kuepusha wananchi Milioni 2.8 wanaokumbwa na njaa. Sasa shirika hilo linahaha kuokoa watoto kupitia mbinu mbali mbali. Je ni njia zipi hizo? Assumpta Massoi anafafanua kwenye makala hii.