Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wamuenzi katibu Mkuu wake wa sita Boutrous Boutrous-Ghali:

UM wamuenzi katibu Mkuu wake wa sita Boutrous Boutrous-Ghali:

Baraza Kuu la Umoja wa mataifa leo limeuwenzi aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa sita wa Umoja wa mataifa Boutrous Boutros-Ghali aliyefariki dunia Jumanne wiki hii akiwa na umri wa miaka 93. Bwana Ghali aliyeingia madarakani mara tuu baada ya vita baridi mchango wake mchango wake utakumbukwa daima katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Amani, demokrasia , mazingira, haki za binadamu zikiwemo za wanawake, maendeleo ya kijamii na changamoto zinazoyakabili mataifa madogo ya visiwani.

Akizungumzia mchango wake Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema kwanza alivuka vikwazo kwa kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Afrika na wa Kiarabu, na siku zote aliwapa sauti masikini na mataifa yasiyojiweza , akiongeza

(SAUTI YA BAN)

Boutros Boutros-Ghali aliusaidia Umoja wa mataifa kuingia katika mazingira mapya.”