Mashambulizi dhidi ya walinda amani hayatapunguza jitihada za Umoja wa Mataifa: Ban

Mashambulizi dhidi ya walinda amani hayatapunguza jitihada za Umoja wa Mataifa: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mashambulizi yaliyotokea leo kwenye kambi ya walinda amani iliyoko Kidal, kaskazini mwa Mali.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric imeeleza kwamba walinda amani wapatao watano wameuawa na wengine 30 wamejeruhiwa.

Bwana Dujarric amemnukuu Katibu Mkuu akisisitiza kwamba mashambulizi dhidi ya walinda amani ni uhalifu wa kivita.

Hata hivyoa amesema ashambulizi dhidi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSMA hayatapunguza utashi wa Umoja huo wa kuisaidia serikali na raia wa Mali katika jitihada zao za kujenga amani ya kudumu na utulivu nchini humo.

Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, akiwatakia nafuu waliojeruhiwa.